Saturday, 21 May 2016

GRANIT XHAKA NDANI!



Aliyekuwa mchezaji wa Borussia Mönchengladbach ambae pia ni raia wa Uswizi Granit Xhaka sasa ni mchezaji rasmi wa Arsenal FC ya Uingereza.

Katika pita pita zetu tumeweza kujipatia picha mpya zaidi ambazo hazijatolewa katika mitandao yeyote zikionyesha Xhaka akipiga picha akiwa amevalia sare za msimu ujao za Klabu ya Arsenal.

Raia huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 23 alitarajiwa kutia sahihi mkataba na The Gunners unaokisiwa kugharimu Pauni Milioni 25 baada ya kutua jijini London siku ya Ijumaa, Mei 20.

Xhaka anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal katika dirisha hili la uhamisho msimu wa kiangazi nchini Uingereza.

Hata hivyo tangazo rasmi la kukamilika kwa uhamisho huo linatarajiwa kutolewa wakati wowte kuanzia sasa.

Friday, 20 May 2016

XHAKA ATUA LONDON!




Ni habari ambayo itawafurahisha mashabiki wengi wa klabu ya Arsenal kote duniani.
Kulingana na mwanahabari Jack Pitt-Brooke wa gazeti la Independent, Granit Xhaka ametua jijini London hii leo kumalizia hatua zake za mwisho kabla ya kuhamia miamba wa kambumbu wa EPL jijini Londo, Arsenal.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye ameibuka kuwa kiungo matata barani Uropa amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kuwa mchezaji wa kwamba kusajiliwa na Klabu hio katika dirisha kubwa la uhamisho nchini humo la msimu wa kiangazi.


Hata hivyo kulitokea taarifa tata kuhusiana na kitita cha pesa ambacho Klabu ya Arsenal iliweka mezani katika majadiliano ya kumnunua mchezaji huyo kutoka klabu yake ya Borussia Mönchengladbach. Laini taarifa hizi kwamba ameshatua jijini London basi zitawapa furaha nyingi mashabiki wa The Gunners.


Mapema wiki hii Xhaka alitaja Klabu ya Arsenal kama klabu ambacho angependa muno kukichezea.
Mashabiki wa Arsenal sasa wanasubiri kwa hamu kuona usajili huo umekamilika huku Xhaka akitarajiwa kuipiga jeki ngome ya kiungo cha kati ya The Gunners.