Aliyekuwa mchezaji wa Borussia Mönchengladbach ambae pia ni raia wa Uswizi Granit Xhaka sasa ni mchezaji rasmi wa Arsenal FC ya Uingereza.
Katika pita pita zetu tumeweza kujipatia picha mpya zaidi ambazo hazijatolewa katika mitandao yeyote zikionyesha Xhaka akipiga picha akiwa amevalia sare za msimu ujao za Klabu ya Arsenal.
Raia huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 23 alitarajiwa kutia sahihi mkataba na The Gunners unaokisiwa kugharimu Pauni Milioni 25 baada ya kutua jijini London siku ya Ijumaa, Mei 20.
Xhaka anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal katika dirisha hili la uhamisho msimu wa kiangazi nchini Uingereza.
Hata hivyo tangazo rasmi la kukamilika kwa uhamisho huo
linatarajiwa kutolewa wakati wowte kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment