Ni habari ambayo itawafurahisha mashabiki wengi wa klabu ya Arsenal kote duniani.
Kulingana na mwanahabari Jack Pitt-Brooke wa gazeti la Independent, Granit Xhaka ametua jijini London hii leo kumalizia hatua zake za mwisho kabla ya kuhamia miamba wa kambumbu wa EPL jijini Londo, Arsenal.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye ameibuka kuwa kiungo matata barani Uropa amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kuwa mchezaji wa kwamba kusajiliwa na Klabu hio katika dirisha kubwa la uhamisho nchini humo la msimu wa kiangazi.
Hata hivyo kulitokea taarifa tata kuhusiana na kitita cha pesa ambacho Klabu ya Arsenal iliweka mezani katika majadiliano ya kumnunua mchezaji huyo kutoka klabu yake ya Borussia Mönchengladbach. Laini taarifa hizi kwamba ameshatua jijini London basi zitawapa furaha nyingi mashabiki wa The Gunners.
Mapema wiki hii Xhaka alitaja Klabu ya Arsenal kama klabu ambacho angependa muno kukichezea.
Mashabiki wa Arsenal sasa wanasubiri kwa hamu kuona usajili huo
umekamilika huku Xhaka akitarajiwa kuipiga jeki ngome ya kiungo cha kati ya The
Gunners.
No comments:
Post a Comment