![]() |
Rihanna |
Msanii wa kike kutoka Marekani mwenye asili ya Barbados, Rihanna haachi
kuzua gumzo kila mara. Hili linatokea akiwa kazini ama hata akiwa kwenye
likizo.
Ijumaa iliyopita alizua hali tete baada yake kuhudhuria mechi ya
mpira wa vikapu jijini New York huku akiwa amevaa kitopu bila sidiria ndani.
![]() |
Rihanna akishabikia Brooklyn Nets |
Tendo hili kidogo lilizua tumbo joto kwenye mechi kati ya Brooklyn Nets na Toronto Raptors baada yake kuketi kwenye safu ya mbele pande ya mashabiki wa Brooklyn Nets
huku chuchu zake zikionekana kupinda na kuwazuzua sio mashabiki wa kiume pekee
bali hata wale wa kike.
Huku akiwa amevaa hipster iliyombana na kuitoa ile figa yake kati,
msanii huyo anayevuma na kazi yake mpya ya ‘Something More’ alionekana kupungwa
na jinsi Brooklyn Nets ilivyowalemea wenzao wa Toronto Raptors kwa vikapu 102
kwa 98.
![]() |
Rihanna akiwa na rafiki wake wa karibu |
Rihanna aliyejumuika na rafiki zake wawili alionekana wakati huo
wote akijiburudisha na kinywaji baridi labda sababu kuu yake ya kuvalia kivazi
kilichoonyesha sehemu cha chuchu zake.
Aidha msanii huyo aliyevuma na kazi yake ya ‘Umbrella’ alionekana
na kipochi kilichochorwa noti ya Dola Mia Moja ya Marekani ambacho
kinakakadiriwa kugharimu Dola 48 za marekani.
![]() |
Rihanna |
Kilichowashangaza wengi aidha ni kutokuwepo kwa mchumba wake,
Drake ambaye kwa siku za hivi majuzi wamekuwa wakiandamana kila sehemu kama mtu
na kivuli chake. Mara ya mwisho ya wawili hao kutokea kwenye umma wakiwa pamoja
ni wiki moja iliyopita walipokwenda kupata chajio kwenye mkahawa wa Madeo eneo la West Hollywood.
Rihanna alizaliwa Februari, 20 mwaka 1988 kama Robyn Fenty katika
Parokia ya St. Michael, Barbados. Alisajiliwa kwenye rekodi za Def Jam akiwa na
umri wa miaka 16 pekee na kwenda kutoa albam yake ya kwanza mwaka wa 2005
iliyouza zaidi ya kopi milioni 2 duniani.
No comments:
Post a Comment