Wednesday, 23 April 2014

P-Square wamaliza ugomvi..?

Habari zilizogonga vichwa barani Afrika na dunia nzima kuhusu ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya mapacha Peter and Paul kutoka nchini Naijeria wanaounda kundi la P-Square na kaka zao ziliwashtua wengi ila hakuna mtu aliyejua kiini cha sakata hio kilikuwa ni nini. Kulingana na chanzo kilichoko karibu na mapacha hao kilitoa sababu kamili ya ugomvi huo.

Chanzo hicho aidha kimedokeza kwamba mgogoro uliletwa na wasaidizi wao wa kibinafsi al maaruf PA’s.
Ukoko ulianza kualika maua pale Msaidizi wa kaka yao mkubwa Jude ajulikanaye kama Wande alimpa Msaidizi wa Peter ajulikanaye kama Shege hela ili akamsajilie gari lake lakini Shege alikosa kufanya hivyo na kuzitumia hela hizo kwa shughuli zingine ambazo hazijabainika.
Baada ya hapo inadaiwa kuwa Msaidizi wa Jude aligadhabishwa muno na tendo hilo la Msaidizi wa Peter.

Jambo hili lilimpeleka nyumbani kwa mapacha hao ijulikanayo kama ‘Squareville’ ili aweze kukabiliana na Msaidizi wa Peter, Shege. Hapo ndipo ngoma ikachukua mwelekeo mbovu.
Mambo yalichachawa pale Peter alipoingilia mzozo huo na kutaka kumpiga Msaidizi wa Jude, Wande. Pale Paul alipojaribu kumkanya, chanzo chetu kinasema Peter alimkandamiza ngumi Paul hadi akaanguka. Paul aidha hakumrudishia ngumi kakake na badala yake kaka yao mwingine anayejulikana kama Tony aliingilia na kuanza kupigana na Peter.

Chanzo chetu aidha kimedai kiini cha vuta n’kuvute hii ni zaidi ya sintofahamu hio na Wasaidizi wao. Aidha inadaiwa kwamba Peter amekuwa akifanya kila awezalo aidha awe mhusika mkuu wa maswala ya kifedha ya kundi la P-Square ama aweze kupata mgao mkubwa zaidi na kwa pande nyingine inadaiwa kwamba Paul anasisitiza kwamba kaka yao mkubwa anayejulikana kama Jude ambaye ni Meneja wa mapacha hao aendelee kuwa Msimamizi wao wa Maswala ya Kifedha.
Kipute hiki kilinuka kiasi ya kwamba ndugu hao walitaka wagawane mali yao ili kitu mmoja aende njia yake.

Lakini baada ya purukushani hii iliyochukua siku kadhaa, Paul alipost hivi katika ukurasa wake wa Facebook.

“After the storm comes calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention”.

Labda hii ni ishara kwamba ndugu hao wameweka tofauti zao za kibinafsi kuhakikisha kwamba jina la P-SQUARE litaendelea kung’aa duniani kama ilivyokuwa.
Sisi hapa Tamashani tunawaombea kila la kheir katika maono yao.



No comments:

Post a Comment