![]() |
P-Square |
Baada ya mitandao ya kijamii nchini Naijeria kuchapisha habari kwamba
mapacha, Peter na Paul wanaounda kundi la P-Square wanataka kutengana kutokana
na kutoelewana, msemaji wa kundi hilo Bayo Adetu amejitokeza na kukanusha madai
hayo.
Akiongea na Premium Times, Adetu alisema hivi na namnukuu,
“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where
that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site.
It’s baseless and untrue.”
Bara zima la Afrika liliamkia habari hizi za kutamausha kuwa mapacha hao
walitofautiana kiasi cha kutaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.
Kuchachawiza habari hizo zaidi, kaka ya P-Square, Jude Okoye ambaye ndie
Maneja wao alitweet akisema,
“After over 10 years of hard work, it’s over. Am
done.”
Wengi walioona hii kuwa ishara kamili kwamba Jude amejitoa kutoka kwa
kundi hilo baada ya kudai kuwa hatohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake
itakayoandaliwa Dubai.
Duru za kuaminika pia zinatuarifu kwamba Jude Okoye hana uhusiano mwema
na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo, jambo ambalo lilimfanya kutohudhuria
harusi yao.
![]() |
P-Square na wake zao |
No comments:
Post a Comment