Msanii Jackson Makini aka Rapcellency aka King Mswati aka Prezzo amekuwa habari ya mjini baada ya kuachilia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina, MY GIRL. Kazi hii mpya aliyoiachilia kwenye mtandao Jumatatu imekuwa gumzo kwenye kanda hii huku wengine wakimpa shavu Prezzo na wengine wakimkashifu kwa kile wanachodai kama kuwadhalalisha dada zetu kutokana na jinsi alivyomtumia Vera Sidika ambaye ana umaarufu wa kuigiza kwenye kanda kadhaa za video kutokana na umbo lake linalowakosesha wanaume wengi usingizi.
Akizungumza na mkali wao Sylva anayesimamia blog hii ya Tamashani kwamba kamwe hajadhalalisha kina dada.
"Kakangu mimi kamwe sijapania kufanya kazi ambazo zitadhalalisha jinsia flani. Kazi hii ni moja ya kazi nilizozitilia bidii sana ili iwe ya kiwango cha kimataifa"
'My Girl' ndio track ya kwanza kwenye album mpya inayokuja itayokwenda kwa jina la Rapcellency.
No comments:
Post a Comment