Kifo chatangazwa
cha sanaa mnayoipenda Hiphop imeshindwa kumaliza calendar
Ni swala ambalo
naamini litazua mitazamo tofauti. Je, mziki aina ya Hip Hop upo ama ushaaga? Ni
swali ambalo limezungumziwa na Msanii wa Hip Hop Jemedari kutoka nchini Kenya
ambaye anasimama na vina vya kina katika kazi yake mpya, R.I.P Hip Hop akisema
kwamba ile real Hip Hop haipo tena duniani. Sikiliza kazi hio kupitia hino link.
https://www.youtube.com/watch?v=XmzyCLEr408
Kama ada yetu
tulimtafuta Jemedari na kutaka kupata kauli yake kuhusiana na na swala hili. Na
hivi na mazungumzo kwa njia ya chat yalivyokuwa.
Sylvano Mbatu
Vipi kaka. Kazi nzuri. Ila naomba
unifafanulie mbona ukaamua kuimba R.I.P Hip Hop.
Unazungumzia nani kwenye beti zako?
Ni utunzi tu ama ni mtu flani
aliyepitia hayo?
Ile 'old' generation ya wasanii ambao
kiasi hawakufanikiwa kama tulivyotarajia
Anhaa
Kwanzia Kshaka na Ukoo Flani kwa
ujumla. Ni kama sanaa ya hiphop ilikufa hapo kiasi..
Hadithi ni kwa ujumla tu lakini ni
career za wasanii weni zimelengwa hapo..
Oh ok
So hivi wataka kuthibitisha kwamba hip
hop imekufa?
Ile "old school" flavour ya
kina Kshaka, kwa mfano, haipo tena..
New cats wamekuja na mitindo tofauti,
ila ni vigumu kupata heshima kutoka kwa hawa wakongwe..
Oh ok
Hino flava mpya ambayo ipo sokoni kwa
sasa, je waeza ipa jina gani? Hip Hop?
Ni hiphop, ile new school.
Kisha kuna Candy Rap, utani kisha
mizani na utunzi mwepesi mno
Kina Camp Mulla, Jay A, na kadhalika..
Anhaa
So huo ndo mtazamo wa msanii Jemedari. Hapa
Tamashani tukisubiri ujio wa kanda ya video ya kazi hii, tutazidi kutafuta
mitizamo kutoka kwa wakali wa Hip Hop kutoka kwenye kanda hii tujue wanafeel
aje.
Jemedari amekuwa katika mstari wa mbele katika kufanya sanaa ya
Hip Hop san asana kwenye njia ya kutumia ala ama Live Performance. Vile vile
amejihusisha na kuandaa tamasha za Hip Hop kama vile Suit n Mics.
No comments:
Post a Comment