Saturday, 21 May 2016

GRANIT XHAKA NDANI!



Aliyekuwa mchezaji wa Borussia Mönchengladbach ambae pia ni raia wa Uswizi Granit Xhaka sasa ni mchezaji rasmi wa Arsenal FC ya Uingereza.

Katika pita pita zetu tumeweza kujipatia picha mpya zaidi ambazo hazijatolewa katika mitandao yeyote zikionyesha Xhaka akipiga picha akiwa amevalia sare za msimu ujao za Klabu ya Arsenal.

Raia huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 23 alitarajiwa kutia sahihi mkataba na The Gunners unaokisiwa kugharimu Pauni Milioni 25 baada ya kutua jijini London siku ya Ijumaa, Mei 20.

Xhaka anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal katika dirisha hili la uhamisho msimu wa kiangazi nchini Uingereza.

Hata hivyo tangazo rasmi la kukamilika kwa uhamisho huo linatarajiwa kutolewa wakati wowte kuanzia sasa.

Friday, 20 May 2016

XHAKA ATUA LONDON!




Ni habari ambayo itawafurahisha mashabiki wengi wa klabu ya Arsenal kote duniani.
Kulingana na mwanahabari Jack Pitt-Brooke wa gazeti la Independent, Granit Xhaka ametua jijini London hii leo kumalizia hatua zake za mwisho kabla ya kuhamia miamba wa kambumbu wa EPL jijini Londo, Arsenal.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye ameibuka kuwa kiungo matata barani Uropa amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kuwa mchezaji wa kwamba kusajiliwa na Klabu hio katika dirisha kubwa la uhamisho nchini humo la msimu wa kiangazi.


Hata hivyo kulitokea taarifa tata kuhusiana na kitita cha pesa ambacho Klabu ya Arsenal iliweka mezani katika majadiliano ya kumnunua mchezaji huyo kutoka klabu yake ya Borussia Mönchengladbach. Laini taarifa hizi kwamba ameshatua jijini London basi zitawapa furaha nyingi mashabiki wa The Gunners.


Mapema wiki hii Xhaka alitaja Klabu ya Arsenal kama klabu ambacho angependa muno kukichezea.
Mashabiki wa Arsenal sasa wanasubiri kwa hamu kuona usajili huo umekamilika huku Xhaka akitarajiwa kuipiga jeki ngome ya kiungo cha kati ya The Gunners.

Sunday, 27 April 2014

Rihanna; jamani ni joto, fesheni ama mitego tu..?

Rihanna 
Msanii wa kike kutoka Marekani mwenye asili ya Barbados, Rihanna haachi kuzua gumzo kila mara. Hili linatokea akiwa kazini ama hata akiwa kwenye likizo.
Ijumaa iliyopita alizua hali tete baada yake kuhudhuria mechi ya mpira wa vikapu jijini New York huku akiwa amevaa kitopu bila sidiria ndani.
Rihanna akishabikia Brooklyn Nets
Tendo hili kidogo lilizua tumbo joto kwenye mechi kati ya Brooklyn Nets na Toronto Raptors baada yake kuketi kwenye safu ya mbele pande ya mashabiki wa Brooklyn Nets huku chuchu zake zikionekana kupinda na kuwazuzua sio mashabiki wa kiume pekee bali hata wale wa kike.
Huku akiwa amevaa hipster iliyombana na kuitoa ile figa yake kati, msanii huyo anayevuma na kazi yake mpya ya ‘Something More’ alionekana kupungwa na jinsi Brooklyn Nets ilivyowalemea wenzao wa Toronto Raptors kwa vikapu 102 kwa 98.
Rihanna akiwa na rafiki wake wa karibu
Rihanna aliyejumuika na rafiki zake wawili alionekana wakati huo wote akijiburudisha na kinywaji baridi labda sababu kuu yake ya kuvalia kivazi kilichoonyesha sehemu cha chuchu zake.
Aidha msanii huyo aliyevuma na kazi yake ya ‘Umbrella’ alionekana na kipochi kilichochorwa noti ya Dola Mia Moja ya Marekani ambacho kinakakadiriwa kugharimu Dola 48 za marekani.
Rihanna
Kilichowashangaza wengi aidha ni kutokuwepo kwa mchumba wake, Drake ambaye kwa siku za hivi majuzi wamekuwa wakiandamana kila sehemu kama mtu na kivuli chake. Mara ya mwisho ya wawili hao kutokea kwenye umma wakiwa pamoja ni wiki moja iliyopita walipokwenda kupata chajio kwenye mkahawa wa Madeo eneo la West Hollywood.


Riri kama anavyofahamika na wendani wake wa karibu yupo jikoni kwa sasa akiandaa albam yake ya nane ya studio ambayo inapikwa na Maprodyusa DJ Mustard, David Guetta na Nicky Romero.
Rihanna alizaliwa Februari, 20 mwaka 1988 kama Robyn Fenty katika Parokia ya St. Michael, Barbados. Alisajiliwa kwenye rekodi za Def Jam akiwa na umri wa miaka 16 pekee na kwenda kutoa albam yake ya kwanza mwaka wa 2005 iliyouza zaidi ya kopi milioni 2 duniani.




Wednesday, 23 April 2014

P-Square wamaliza ugomvi..?

Habari zilizogonga vichwa barani Afrika na dunia nzima kuhusu ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya mapacha Peter and Paul kutoka nchini Naijeria wanaounda kundi la P-Square na kaka zao ziliwashtua wengi ila hakuna mtu aliyejua kiini cha sakata hio kilikuwa ni nini. Kulingana na chanzo kilichoko karibu na mapacha hao kilitoa sababu kamili ya ugomvi huo.

Chanzo hicho aidha kimedokeza kwamba mgogoro uliletwa na wasaidizi wao wa kibinafsi al maaruf PA’s.
Ukoko ulianza kualika maua pale Msaidizi wa kaka yao mkubwa Jude ajulikanaye kama Wande alimpa Msaidizi wa Peter ajulikanaye kama Shege hela ili akamsajilie gari lake lakini Shege alikosa kufanya hivyo na kuzitumia hela hizo kwa shughuli zingine ambazo hazijabainika.
Baada ya hapo inadaiwa kuwa Msaidizi wa Jude aligadhabishwa muno na tendo hilo la Msaidizi wa Peter.

Jambo hili lilimpeleka nyumbani kwa mapacha hao ijulikanayo kama ‘Squareville’ ili aweze kukabiliana na Msaidizi wa Peter, Shege. Hapo ndipo ngoma ikachukua mwelekeo mbovu.
Mambo yalichachawa pale Peter alipoingilia mzozo huo na kutaka kumpiga Msaidizi wa Jude, Wande. Pale Paul alipojaribu kumkanya, chanzo chetu kinasema Peter alimkandamiza ngumi Paul hadi akaanguka. Paul aidha hakumrudishia ngumi kakake na badala yake kaka yao mwingine anayejulikana kama Tony aliingilia na kuanza kupigana na Peter.

Chanzo chetu aidha kimedai kiini cha vuta n’kuvute hii ni zaidi ya sintofahamu hio na Wasaidizi wao. Aidha inadaiwa kwamba Peter amekuwa akifanya kila awezalo aidha awe mhusika mkuu wa maswala ya kifedha ya kundi la P-Square ama aweze kupata mgao mkubwa zaidi na kwa pande nyingine inadaiwa kwamba Paul anasisitiza kwamba kaka yao mkubwa anayejulikana kama Jude ambaye ni Meneja wa mapacha hao aendelee kuwa Msimamizi wao wa Maswala ya Kifedha.
Kipute hiki kilinuka kiasi ya kwamba ndugu hao walitaka wagawane mali yao ili kitu mmoja aende njia yake.

Lakini baada ya purukushani hii iliyochukua siku kadhaa, Paul alipost hivi katika ukurasa wake wa Facebook.

“After the storm comes calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention”.

Labda hii ni ishara kwamba ndugu hao wameweka tofauti zao za kibinafsi kuhakikisha kwamba jina la P-SQUARE litaendelea kung’aa duniani kama ilivyokuwa.
Sisi hapa Tamashani tunawaombea kila la kheir katika maono yao.