Sunday, 27 April 2014

Rihanna; jamani ni joto, fesheni ama mitego tu..?

Rihanna 
Msanii wa kike kutoka Marekani mwenye asili ya Barbados, Rihanna haachi kuzua gumzo kila mara. Hili linatokea akiwa kazini ama hata akiwa kwenye likizo.
Ijumaa iliyopita alizua hali tete baada yake kuhudhuria mechi ya mpira wa vikapu jijini New York huku akiwa amevaa kitopu bila sidiria ndani.
Rihanna akishabikia Brooklyn Nets
Tendo hili kidogo lilizua tumbo joto kwenye mechi kati ya Brooklyn Nets na Toronto Raptors baada yake kuketi kwenye safu ya mbele pande ya mashabiki wa Brooklyn Nets huku chuchu zake zikionekana kupinda na kuwazuzua sio mashabiki wa kiume pekee bali hata wale wa kike.
Huku akiwa amevaa hipster iliyombana na kuitoa ile figa yake kati, msanii huyo anayevuma na kazi yake mpya ya ‘Something More’ alionekana kupungwa na jinsi Brooklyn Nets ilivyowalemea wenzao wa Toronto Raptors kwa vikapu 102 kwa 98.
Rihanna akiwa na rafiki wake wa karibu
Rihanna aliyejumuika na rafiki zake wawili alionekana wakati huo wote akijiburudisha na kinywaji baridi labda sababu kuu yake ya kuvalia kivazi kilichoonyesha sehemu cha chuchu zake.
Aidha msanii huyo aliyevuma na kazi yake ya ‘Umbrella’ alionekana na kipochi kilichochorwa noti ya Dola Mia Moja ya Marekani ambacho kinakakadiriwa kugharimu Dola 48 za marekani.
Rihanna
Kilichowashangaza wengi aidha ni kutokuwepo kwa mchumba wake, Drake ambaye kwa siku za hivi majuzi wamekuwa wakiandamana kila sehemu kama mtu na kivuli chake. Mara ya mwisho ya wawili hao kutokea kwenye umma wakiwa pamoja ni wiki moja iliyopita walipokwenda kupata chajio kwenye mkahawa wa Madeo eneo la West Hollywood.


Riri kama anavyofahamika na wendani wake wa karibu yupo jikoni kwa sasa akiandaa albam yake ya nane ya studio ambayo inapikwa na Maprodyusa DJ Mustard, David Guetta na Nicky Romero.
Rihanna alizaliwa Februari, 20 mwaka 1988 kama Robyn Fenty katika Parokia ya St. Michael, Barbados. Alisajiliwa kwenye rekodi za Def Jam akiwa na umri wa miaka 16 pekee na kwenda kutoa albam yake ya kwanza mwaka wa 2005 iliyouza zaidi ya kopi milioni 2 duniani.




Wednesday, 23 April 2014

P-Square wamaliza ugomvi..?

Habari zilizogonga vichwa barani Afrika na dunia nzima kuhusu ugomvi ulioibuka wiki iliyopita baina ya mapacha Peter and Paul kutoka nchini Naijeria wanaounda kundi la P-Square na kaka zao ziliwashtua wengi ila hakuna mtu aliyejua kiini cha sakata hio kilikuwa ni nini. Kulingana na chanzo kilichoko karibu na mapacha hao kilitoa sababu kamili ya ugomvi huo.

Chanzo hicho aidha kimedokeza kwamba mgogoro uliletwa na wasaidizi wao wa kibinafsi al maaruf PA’s.
Ukoko ulianza kualika maua pale Msaidizi wa kaka yao mkubwa Jude ajulikanaye kama Wande alimpa Msaidizi wa Peter ajulikanaye kama Shege hela ili akamsajilie gari lake lakini Shege alikosa kufanya hivyo na kuzitumia hela hizo kwa shughuli zingine ambazo hazijabainika.
Baada ya hapo inadaiwa kuwa Msaidizi wa Jude aligadhabishwa muno na tendo hilo la Msaidizi wa Peter.

Jambo hili lilimpeleka nyumbani kwa mapacha hao ijulikanayo kama ‘Squareville’ ili aweze kukabiliana na Msaidizi wa Peter, Shege. Hapo ndipo ngoma ikachukua mwelekeo mbovu.
Mambo yalichachawa pale Peter alipoingilia mzozo huo na kutaka kumpiga Msaidizi wa Jude, Wande. Pale Paul alipojaribu kumkanya, chanzo chetu kinasema Peter alimkandamiza ngumi Paul hadi akaanguka. Paul aidha hakumrudishia ngumi kakake na badala yake kaka yao mwingine anayejulikana kama Tony aliingilia na kuanza kupigana na Peter.

Chanzo chetu aidha kimedai kiini cha vuta n’kuvute hii ni zaidi ya sintofahamu hio na Wasaidizi wao. Aidha inadaiwa kwamba Peter amekuwa akifanya kila awezalo aidha awe mhusika mkuu wa maswala ya kifedha ya kundi la P-Square ama aweze kupata mgao mkubwa zaidi na kwa pande nyingine inadaiwa kwamba Paul anasisitiza kwamba kaka yao mkubwa anayejulikana kama Jude ambaye ni Meneja wa mapacha hao aendelee kuwa Msimamizi wao wa Maswala ya Kifedha.
Kipute hiki kilinuka kiasi ya kwamba ndugu hao walitaka wagawane mali yao ili kitu mmoja aende njia yake.

Lakini baada ya purukushani hii iliyochukua siku kadhaa, Paul alipost hivi katika ukurasa wake wa Facebook.

“After the storm comes calm. Hoping for better days ahead as one family. God’s intervention”.

Labda hii ni ishara kwamba ndugu hao wameweka tofauti zao za kibinafsi kuhakikisha kwamba jina la P-SQUARE litaendelea kung’aa duniani kama ilivyokuwa.
Sisi hapa Tamashani tunawaombea kila la kheir katika maono yao.



Sunday, 20 April 2014

Niacheni Nidate’ asema Raz a.k.a Raz Swagg Level..!

Raz
Msanii wa kizazi kipya Raz a.k.a Raz Micha aitwavyo akiwa mtaani aonyesha kila sababu ya kwa nini yeye ni mojawapo ya wasanii wanaongoza fani ya mziki wa kizazi kipya kutoka Pwani ya Kenya baada ya kuachilia pini jipya na bonge la video linalokwenda kwa jina ‘Niache Nidate’.
Raz akiwa na Marie kwenye shoot ya 'Niache Nidate'

Kazi hio ilifuatiliwa na kuachiliwa sokoni kwa video kali iliyofanywa na muongozaji namba moja wa video eneo la Pwani ya Kenya Lil Guy G, video ambayo imeshirikisha wakali kibao wa kazi hizi kama vile, Ally Kiba, Sylvano Mbatu (Mkurugenzi wa Tamashani), Bob Junior a.k.a Sharobaro President na Bonge la Nyau kutoka nchini Tanzania bila kusahau mtoto wa kike Marie aliyeigizia kwenye kanda hio ambaye ni bonge la actress kwenye vipindi aina aina humu nchini.
Raz akila bata pamoja na Ally Kiba


Akizungumza na meza ya Tamashani, Raz ambaye majina yake rasmi ni Rama Sultan alihoji kwamba aliwekeza kitita kikubwa cha fedha kuhakikisha kwamba kazi hio imekubalika kwenye kanda hii.

Fidempa(kushoto), Prodyusa Totti pamoja na Raz wakiwa jikoni
Raz ameweza kutamba anga zake kama msanii mwenye umri mdogo ila mwingi wa ujuzi na ufundi... Hili limemwezesha kufanya kazi na wasanii kama vile Ally Kiba kwenye ‘Mjanja wa Jiji’, Hakim5 kwa 'Nidanganye', J.I kwenye 'Dini', Chikuzee, AT kwenye track 'Sina Habari na Mtu', CLD, Fidempa kwenye track ya 'Swagger Up', Lil Kizzy kutoka Germany, Wizzy A kutoka Naijeria na wasanii wengine kwenye kanda hii.

Sylva(Meneja wa Tamashani), Babyone(Msanii kutoka Sudan Kusini) pamoja na Raz.
Licha ya hayo bado ana maono kufanya kazi zingine kubwa na wasani tofauti wa kimataifa maana ana maono makubwa na kazi yake ..

Kwa sasa hapa Tamashani tunamtakia kila la Kheri na tunampa Raz nafasi ya Kudata maana wakati wake ndio sasa.

Saturday, 19 April 2014

P-Square yasambaratika..?


P-Square



Baada ya mitandao ya kijamii nchini Naijeria kuchapisha habari kwamba mapacha, Peter na Paul wanaounda kundi la P-Square wanataka kutengana kutokana na kutoelewana, msemaji wa kundi hilo Bayo Adetu amejitokeza na kukanusha madai hayo.

Akiongea na Premium Times, Adetu alisema hivi na namnukuu,

“I am too busy to give some wanna be blogger traffic, I don’t know where that report is coming from. Maybe they just want to get traffic to their site. It’s baseless and untrue.”
 
P-Square

Bara zima la Afrika liliamkia habari hizi za kutamausha kuwa mapacha hao walitofautiana kiasi cha kutaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.
 
P-Square wakiwa na kaka yao mkubwa na Maneja Jude Okoye
Kuchachawiza habari hizo zaidi, kaka ya P-Square, Jude Okoye ambaye ndie Maneja wao alitweet akisema, 

“After over 10 years of hard work, it’s over. Am done.”

Wengi walioona hii kuwa ishara kamili kwamba Jude amejitoa kutoka kwa kundi hilo baada ya kudai kuwa hatohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake itakayoandaliwa Dubai.
Duru za kuaminika pia zinatuarifu kwamba Jude Okoye hana uhusiano mwema na mke wa Peter Okoye, Lola Omotayo, jambo ambalo lilimfanya kutohudhuria harusi yao.


 
P-Square na wake zao